|
Katika ukurasa huu utaona MIGOGORO, ASILI NAAINA YAKE, na NJIA ZA
KUITATUA
Lengo kuu la mada
Lengo kuu la mada
hii ni kuwawezesha wadau katika maswala ya Amani,kutafakari juu ya
utambuzi,mitizamona na tabia inayohusiana na migogoro katiak jamii
Utangulizi
Migogoro katika
jamii ni jambo la kawaida kwa sababu ni sehemu ya maisha ya binadamu
.migogoro hutokea kwa sababu kila mtu kwa ubinafsi wake ni tofauti
na mwenzake, hivyo kila mtu ana vitu anavyovithamini , ana mahitaji
binafsi na shauku binafsi .
1.1: MAANA YA MIGOGORO
migogoro maana
yake ni vurugu au makabiliano ya silaha ya ana kwa ana au mapambano
baina ya vikundi au kikundi, au baina ya dola na dola au madola .katika
makabiliano au mapambano hayo watu wanaohusika hujeruhiwa na wengine
huuawa
Neno migogoro
hutumika vilevile kumahanisha vita ya kiraiya, ugomvi WA kiraiya
{civil strife,uhasama vita,na udhaifu wa kisiasa{political
instability}
1.2:CHANZO/ASILI YA MIGOGORO
Chanzo cha
migogoro hutofautiana kutokana na sehemu na sehemu na aina ya
migogoro husika . Hata hivyo asili hasa ya migogoro ni tofauti
zinazotokana na ubinafsi, mahitaji na shauku za kila binadamu.
1.3:AINA YA MIGOGORO
. Migogoro ya
mipaka
.Vita vya
kiraiya na migogoro ya ndani yenye kuleta athari kimataifa
.Migogoro
inayotokana na urithi wa madaraka {succession}
.Migogoro ya
kisiasa na kiitikadi
.Migogoro
inayotokana na ufugaji wa kuhamahama
vile vile kuna
migogoro ya kisiasa na vurugu za mjini na vijijini
Migogoro ya
kisiasa ni kama :vita baina ya nchi na nchi,vikund vya waasi ya
dola {serikali}, mapinduzi ya kijeshi na vikundi vinavyojitenga na
waasi
Vurugu au migogoro
ya mijini {Arban violence}Hizi zinaweza kuchukuwa sura ya migogoro
ya kikabila, dini au tabaka {masikini wakivamia mali za serikali,au
maduka na nyumba za matajiri na wakulima }
Migogoro ya
vijijini {Rural Conflict }Hii huwa ni Migogoro ya kikabila hasa
kati ya wafugaji na wakulima.
.Tofauti kati
ya migogoro ya kisiasa na migogoro ya mjini na vijijini ni kwamba
migogoro ya kisiasa dola uhusika kwa namna moja au nyingine migogoro
ya mjini na vjijini dola linaweza lisiwe na wakati mwingine
matukio hayalipotiwi.
.Mijgogoro
kati ya nchi na nchi: Hii mara nyingi ilitokana na mipaka ya
kikoloni
Migogoro ya ndani
Hii ni ya aina
nyingi:
.Ile ambayo
dola ni sehemu ya migogoro, hii uchochewa na siasa
.Migogoro
baina ya vikundi ambavyo dola ni sehemu yake mfano,uasi dhidi ya
serikali iliyoko madarakani, uasi wa kujitenga {secessionist
rebellion}
. mapinduzi
ya kijeshi
.Migogoro
iliyotokana na vita baridi
.Migogoro
ya vina yotokana na vikundi vingi kuwa na huchu wa kuongoza nchi.
. migogoro
ya vijijini kuhusiana na rasilimali.
.vurugu na
migogoro ya mjini.
1.4: SABABU ZA KUWEPO MIGOGORO
A. Siasa
.Kugombania
madaraka ya kuongoza dola
.Uongozi
usio na mwono {vision} na ushawishi toka nje
.Kutokuwa
na uwazi pamoja na uongozi mmbaya
.Uvunjaji
wa haki za binadamu
b. Uchumi :
.
umasikini
.ugawaji
mbovu wa rasilimali na pato la la taifa
.Athari
za mzingo wa deni lanje na mfumo mbaya wa fedha kimataifa
C. Kijamii na
Kitamaduni
.
Tofauti za kitabaka katika jamii
. Mfumo
unaoendekeza utengano katika jamii na huasama wa kikabila
.
Wajibu wanasiasa katika kusikiliza hisia za kikabila na kikanda
.Tofauti
za kitamaduni na kiutafuta utambulisho
. Mfumo
mbaya wa Elimu.
1.5:HATUA ZA MIGOGORO
1.5.1:migogoro
kabla ya ukoloni
Migogoro
mingi iliusu vita kati ya himaya moja na nyingine, uasi wa ndani
dhidi ya watawala, kuzuiya biashara ya watumwa,migogoro baina ya
makabila juu ya malisho,mifugo, ardhi,mauaji ya kulipiza kisasi n.k.
1.5.2:Migogoro
wakati wa ukoroni
Mchakato wa kuiivamia Afrika ulisababisha jamii za kiafrika
kupinga.Hivyo waafrika waliingia vitani kutegemea maendeleo ya
sehemu husika hata pale waafrika waliposhindwa na kuwa chini ya
himaya ya wakoloni migogoro iliendelea kutokana na mabadiliko
yaliyo letwa na wakoloni kama kumiliki ardhi kwa watu binafsi,
kodi,shelia mpya n.k.Hivi vyote vilipingwa na vilisbbisha migogoro.
1.5.3:Migogoro
wakati wa uhuru {1960-2000}
Hii imegawanyika
sehemu tatu:
Kipindi cha
serikali za kizalendo
Kipindi cha vita baridi {1970-1989}
Hiki kilikuwa ni
kipindi ambacho nchi nyingi za Afrika uchumi wa ke ulidumaa.
Mashirika makubwa
ya Fedha duniani WB naIMFyalianza kutunga sera za kiuchumi
Kwa nchi zilizo
kuwa zinaendelea. Sera hizo zilizibana sana nchi za dunia ya tatu na
kusababisha kuongezeka kwa tabaka kati ya wenye nacho na wasiokuwa
nacho.
Migogoro baada ya
vita baridi {1990-2000}:Baada ya vita baridi mabadiliko mengi
yametokea,na ambayo yamesababisha migogoro kuongezeka:
.Wajibu wa WB
na IMF na masharti ya kisiasa kati ya wakopeshaji na wakopaji
wameongezeka.
.Jumuia za
kijamii ndani na nje ya nchi zinazoangalia rekodi za utawala bora na
haki za binadamu katika nchi zimeongezeka
.Athari za SAP
katika kuongeza umaskini mijini na vijijini na kuongezeka kwa idadi
ya watu kumeleta mvutano na migogoro ya rasilimari(ardhi ya kulima/maji
n.k)
.Upatikanaji wa
siraha ndogondogo kutoka kwa wauzaji wa kimataifa na vikundi vya
waasi umeongezeka.
.Utandawazi na
biashara ya kimataifa/mikopo yenye masharti magumu,utegemezi wa
wawekezaji wa nje na uchumi usio shindani kwa nchi nyingi za
kiafrika vimeongezeka.
.Misaada kwa
serikali zilizokuwa za kidikteta(ya kifedha na siraha)vimeondolewa.
.2.0;NJIA ZA
KUONGOZA NA KUTATUA MIGOGORO(Conflict management and
resolution)
Njia zifuatazo
zaweza kutumika pale penye migogoro ili kukabiliana nayo na kuitatua.
.Kuwa na baraza
la usuluishi;Hili linatakiwa kuundwa na watu wenye busara kutoka
pande mbalimbali za nchi na kanda mbalimbali za wananchi.
.Mpatanishi
kutoka nje ya nchi.
.Kuwa na mfumo
bora wa utoaji haki.
.Kuwa na
mawasiliano mazuri.
3.0;JINSI YA
KUBADILI MIGOGORO(Tranforming conflicts)
Ili kubadili
sura ya mgogoro,Pande husika yabidi ifanye mambo yafuatayo;
.Pande
zinazohusika kuwa na maandalizi ya kutosha ya b inafsi.
.Pande zinazo
husika kuwa na
makubaliano
ya kukutana (Zikubaliane mchakato wa kumaliza mgogoro,kukaa
katika meza
ya maeleano,kukubali kuheshimiana,kusiwepo kulaumiana wala
kunyanyuliana vidole,kuwepo na uwazi)
.Pande husika
zielezee shauku na malengo yao ya mwanzo(mfano uzoefu wao jinsi
mgogoro ulivyowaathiri)
.Pande zinazo
husika zizidi kuelezea tena shauku na malengo yao(chukua muda wa
kutafakari yaliosemwa na mwenzako,ukichukua vitu vya msingi)
.Mkubaliane
katika baadhi ya maelezo.
.Endeleeni
kuleta shauku zenu,nafasi na hisia na anzeni kutafuta
ufumbuzi(katika hili ni muhimu kuwa wawazi,kuainisha vitu vya
msingi,mbinu,maeneo mnayokubaliana na msiyokubaliana,jitahidi katika
vitu halisi vinavyoweza kupimika).
.Fanyeni
majumuisho ya makubaliano na mtoe suluhisho.
.Fatilia
(follow up)kuangalia kama suluhisho la mgogoro linatekelezwa na
uangalie tena kama unaona inafaa.
4.0;UZUIAJI
WA MIGOGORO(Prevention of conflicts).
Ili kuzuia
migogoro yatubidi;
1:Kujenga
taifa(National buiding):Watu wanatakiwa wajenge na kuendeleza taifa
kwa kuwa na sera za kiutamaduni zitakazotekelezwa na mfumo wa elimu.
11:Mfumo wa
siasa(Political system):Kuna umuhimu wa kujenga mfumo wa siasa
unaruhusu ushindani katika kugombea kupata madaraka ambayo inaruhusu
vikundi vingine kupata madaraka katika muda muafaka.Mfumo uwaruhusu
watu na vikundi vingine kushiriki katika kuchagua/uchaguzi wa
kumpata mtu au watu ambao wanashiriki katika utoaji wa maamuzi
katika ngazi mbalimbali za madaraka.Vilevile mfumo wa siasa ni
lazima uzingatie mambo haya:
.Kukabidhi ,madaraka
kwa wengine kwa amani.
.Kujilimbikizia
mali kwa kutumia taasisi za serikali au dola kusiruhusiwe maadili ya
utawala bora na demokrasia uzingatiwe(Kuwepo na
uwazi,uwajibikaji,mfumo huru wa haki na sheria,na jeshi liwe la
wananchi).
.Vikundi vya
kijamii vihusishwe katika kuangalia utekelezaji wa sera na utoaji wa
huduma.
111:Ukuaji wa
uchumi(Economic development):Rasilimari za taifa zigawanywe sawa
kati ya kanda na vikundi katika nchi.
1.5:MBINU ZA
MAWASILIANO ZINAWEZA KUSAIDIA KATIKA KUBADILISHA MIOGORO.
.Uwazi
.Uvumilivu
.
.kuheshimiana.
.Uwezo wa
kuhisi maono ya wengine(empathy).
.Maelewano.
|